Date |
Event |
1921 |
Kundi la kwanza la Wamisionari wakapuchini (Gabriel Zelger, Costantine Egger, Stephan Brogle, Guido Kappeli, Allexander Hanggi, Clemens Studer, Jakob Stalder, Franz Xaver Frei) wawasili Dar es salaam. |
1923 |
Ndugu Gabriel Zelger awekwa wakfu kuwa Askofu wa kanda ya Dar es salaam (Mahenge, Ifakara na sehemu za Dodoma na Iringa) |
1923 |
Ndugu wa Provinsia ya Uswisi waungwa mkono na ndugu toka Provinsia za Austria kufanya umisionari Tanzania. Ndugu Johannes B. Bauer toka Provinsia ya Tirol Kaskazini (Austria) aliwasili mwaka 1923. Alifuatiwa na ndugu Franz Seraph Leitner (kutoka Provinsia ya Tirol Kaskani mwaka 1932). Mwaka 1959 waliungwa mkono na Ndugu wawili; Fidelis Krautsack na Ndugu Seraphin Wiesinger kutoka Provinsia ya Viena (Austria). |
1925 |
Mwanzo wa Usekulari (Perpetual Tertiary) Tanzania. Ndugu Rafael Malizani awa Msekulari wa kwanza kupata nadhiri za daima. |
1930 |
Ndugu Edgar Maranta awekwa wakfu kuwa askofu wa kanda ya Dar es Salaam baada ya kustaafu kwa Ndugu Gabriel Zelger (1929). Alipa kipaumbele wazo la kuzalisha mapadri wazawa kwa ajili ya jimbo zaidi kuliko wazo la kueneza shirika. |
17.2.1948 |
Askofu Edgar Maranta na Provinsiali wa Uswisi (Franz Solan Schaeppi) wawekeana mkataba kuanzisha nyumba ya Shirika (Domus Religiosa). Sali yafanywa Domus Religiosa ya kwanza ya Wakapuchini Tanzania. Yawa pia kituo kikuu cha kulea Wasekulari. Sheria za kanisa mahalia hazikuruhusu wajiunge na shirika la Wakapuchini licha ya wengi wao kuonesha nia. |
1948 |
Br. Alfred Lawrence Menezes awa mzalendo wa kwanza (toka katika jamii ya Wagoa walioishi Tanzania) kukubaliwa kujiunga na Novisiati huko Luzern (1948/49). Alifuatiwa na Br. Dunstan Gilbert Dias na Br. Fernando Lawrence de Noronha (1953/1954). Walifanikiwa kupata ukasisi na kuwa wanashirika katika Provinsia ya Uswisi. |
29.8.1949 |
Superior Regularis Gustav Nigg ahamia Domus Religiosa ya Sali. |
1954 |
Askofu Edgar Maranta aendelea kukosoa pendekezo la uanzishwaji wa nyumba ya malezi kwa ajili ya Shirika la Wakapuchini Tanzania. Apendekeza watakaji wapelekwe novisiati Uswisi. |
7.9.1954 |
Br. Joseph Cupertin Mukasa, Msekulari aliyeishi Domus Religiosa ya Sali, akubaliwa kuanza Novisiati huko Luzern. Aweka nadhiri za kwanza 8.9.1955 huko Luzern na za daima huko Sali (1959). Aliacha shirika 1963. Alifuatiwa na ndugu Leonard Mutahya (1960); alianza Novisiati Uswisi na baada ya muda alirudi Tanzania na kuacha shirika. |
15.02.1955 |
Ndugu Matern Marty afariki na baadaye kuzikwa huko Kwiro Mahenge. Kumbukumbu zinashuhudia kwamba Ndugu huyu alikuwa na mangamuzi makubwa sana kiroho. Amehusishwa na kutendeka kwa miujiza mingi. Wengi wanafanya maombezi kupitia Ndugu huyu na juhudi zinafanyika kutambulisha utakatifu wake kwa waamini. |
1959 |
Machafuko ya kisiasa huko Indonesia yaleta chuki dhidi ya raia wa Uholanzi; yapelekea mbadilishano wa wamisionari: wamisionari waholanzi waja Tanzania na baadhi ya Waswisi wahamia Indonesia. |
1959 |
Azimio la mwisho juu ya uundaji wa jamaa ya kwanza ya kizalendo ya kikapuchini lapitishwa huko Uswisi. Nyumba za malezi ya wakandindati na wanovisi zaandaliwa. Mwanzo wa Wakapuchini kusambaa nje ya eneo la Mahenge na Dar es salaam. |
1961 |
Nyumba ya malezi Kasita (Wakandidati, Wapostulanti na wanovisi) yafunguliwa. Agenda ya upanuzi wa shirika yatiliwa mkazo; mwanzo wa Wakapuchini kusambaa majimbo ya Bukoba na Moshi. |
1961 |
Wakandidati wa kwanza (Wasekulari waliolelewa katika Domus Religiosa ya Sali) (Pascal Mkulikuli, Camilius Kavishe, Robert Kyaduma, Gaudenz Mangochi na Optat Ramadhani) wapokelewa kwa kipindi cha Malezi Kasita. Waungwa mkono na Oswald Likwawa, Joseph Shaurimbele na Theofil Pankraz toka Luhombero na Johann Mwani toka Mpanga. |
15.4.1961 |
Ndugu Paskal Mkulikuli, Camillus Kavishe, Felix Likwawa na Chrispin Optat wapokelewa kwa kipindi cha Unovisi huko Kasita. |
24.4.1962 |
Kundi la kwanza la ndugu wazalendo; Br. Camilius Kavishe, Paskali Mkulikuli na Br. Felix Likwawa wafunga nadhiri za kwanza. |
1963 |
Provinsia ya Tuscana yakubali Misioni katika jimbo la Dodoma. Waanza kazi katika wilaya ya Mpwawa. |
1965 |
Provinsia ya Bologna yawatuma ndugu Fidelis Versari na Costanzo Perazzini (na baadaye ndugu Pius Cesare Giorgi and Adriano Gattei) kusaidia umisionari Tanzania. |
1965 |
Shirika laendelea kupanuka nje ya majimbo ya Dar es Salaam na Mahenge. Ndugu waalikwa Bukoba na kutoa malezi kwa mabradha wa jimbo hilo. |
1966 |
Ndugu kutoka Provinsia za India wawasili kwa ajili ya Umisionari Tanzania. Ndugu Gregory Vas (Provinsia ya Utatu Mtakatifu) na Ndugu Abel Thekkekut (Provinsia ya Mt. Yosef) wawasili Tanzania kwa ajili ya umisionari. Kabla yao alitangulia Ndugu Joseph Pais kutoka Provinsia ya Utatu Mtakatifu 1959. |
1969 |
Askofu Edgar Maranta ajiuzulu; Nafasi yake yachukuliwa na Askofu Laurean Rugambwa. |
1970 |
Seminari ndogo ya Maua yafunguliwa rasmi huko Moshi Kilimanjaro. |
1972 |
Malezi ya Wakandidati yahama toka Kasita na kupelekwa Kilolero. |
1977 |
Mlipuko wa ugonjwa wa Malale huko Kilolero wapelekea uhamishwaji wa nyumba ya Malezi ya Wakandidati (Wapostulanti I) kwenda Sofi. |
1979 |
Kufunguliwa kwa nyumba ya Jangwani: yaanza kutumika kama nyumba ya Juniorate hadi 1989. |
1980 |
Ndugu Angelo Simmoneti toka Provinsia ya Toscana aanza mpango wa ujenzi wa kituo cha kuwasaidia watoto walemavu huko Mlali. Ndugu Angelo alifariki tarehe 13.9.1997 |
1981 |
Ndugu Wakapuchini wazidi kukua na kufikia hatua ya General Vice-Province; wamisionari wa nchi zote wawekwa chini ya kiongozi mmoja (Vice-Provincial). |
1985 |
Nyumba ya Wakandidati (Wapostulanti I) yahamishwa toka Sofi kuja Kilomeni. |
1989 |
Malezi ya Junorate yahamia Kola. Malezi ya Wapostulanti (II) yahama toka Kasita kwenda Jangwani-Ifakara. |
1992 |
Ndugu Wakapuchini Tanzania waenda utume visiwa wa Comoro. |
7.6.1994 |
Ndugu Fidelis Versari afariki Dunia. Alisaidia sana katika ujenzi wa Kituo cha Kiroho Mbagala na Shule ya Mtakatifu Anthony Mbagala. |
1996 |
Vice-Provinsia ya Tanzania yatangazwa Provinsia |
1998 |
Provinsia ya Tanzania yatia saini fraternal Memorandum of Agreement na Vice Provinsia ya Africa Kusini na tarehe 16.8.1998 Ndugu Pius Nkilagomva na Odilo Mroso watumwa kuanza umisionari Africa Kusini. |
1999 |
Ndugu Beatus Kinyaiya achaguliwa Provinsiali wa kwanza mzalendo Tanzania. |
16.05.1999 |
Ndugu Thaddaeus Ruwa’ichi awekwa wakfu kuwa askofu Jimbo Katoliki Mbulu. |
Sept 1999 |
Kituo cha Wakandidati chahama toka Kilomeni na kwenda Miyuji. |
02.07.2006 |
Ndugu Beatus Kinyaiya awekwa wakfu kuwa askofu Jimbo Katoliki Mbulu. |
18.8.2009 |
Mkutano wa kwanza wa Mikeka Provinsia ya Tanzania waanza huko Mbagala. |
24.3.2010 |
Ndugu wa Provinsia ya Tanzania warudi tena Afrika Kusini kwa ajili ya umisionari. |
2014 |
Mwanzo wa Fraternal Collaboration kati ya Tanzania na Papua New Guinea. Ndugu Modest Massawe na Ndugu Joseph Kiagho watumwa kwa umisionari PNG. |
2017 |
Kituo cha Wakandidati chahama toka Miyuji kwenda Mlali Kituo. |
15.7.2020 |
Provinsia ya Tanzania yakabidhiwa rasmi jukumu la kuiangalia Custodia ya Malawi. |
2022 |
Kuanza utume katika majimbo ya Sumbawanga na Kigoma. |
2023 |
Kuanza utume katika jimbo la Lindi parokia ya Kipatimu na Mnazi Mmoja. |
Nov 2023 |
Mkutano wa Pili wa Mikeka |